Benjamin Mendy amepatikana hana hatia katika mashtaka saba kati ya tisa dhidi yake. Baada ya kesi iliyochukua takriban miezi mitano, beki huyo wa Manchester City amefutiwa mashtaka sita ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono. Hata hivyo, baada ya siku 13 za mashauriano katika Mahakama ya Chester Crown, mahakama imeshindwa kufikia uamuzi wa mashtaka…

Abdallah Shaibu, anayejulikana pia kama “Ninja,” beki wa kati wa Yanga SC, alirejea baada ya mkataba wake wa mkopo na Dodoma Jiji kumalizika. Tangu wakati huo amejiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya mazoezi Kigamboni, Uwanja wa Avic Town jijini Dar es Salaam. Wakati timu hiyo ikifanya mazoezi ya jana uwanjani hapo, Ninja aliungana nao…

KIUNGO mpya wa klabu hiyo, Saido Ntibazonkiza, anatarajiwa kuanza kuichezea Simba SC kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons, ingawa huenda klabu hiyo ikatoa taarifa ya mchezaji mpya iliyemnunua katika dirisha fupi lililofunguliwa. Endapo kila kitu kitaenda sawa na mipango Ntibazonki atakuwa kiungo wa timu itakayoshuka uwanjani kuwakabili Maafande wa Prisons kwa…

Rais wa Yanga SC Hersi Said leo ameongea kwa mara ya kwanza kuhusu sare ya 0-0 ya Yanga SC dhidi ya Club Africain ya Tunisia ukiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika uliyochezwa November 2 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa. Hersi ameomba radhi mashabikiwa Yanga SC na…

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza Kijana Majaliwa Jackson aliyehusika kuwaokoa Watu 24 kwenye ajali ya ndege iliyotokea Bukoba siku jana atafutiwe kazi kwenye Jeshi la Uokozi. Agizo hilo lililotolewa na Rais Samia kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambapo ameagiza Kijana Majaliwa Jackson akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani…