Haaland hayuko katika ubora wake Pep Guardiola anaamini Erling Haaland hayuko katika kiwango bora licha ya Mnorwei huyo kufunga mabao mawili katika ushindi dhidi ya Leeds Jumatano usiku. Haaland, 22, alikua mchezaji mwepesi zaidi kufunga mabao 20 kwenye Premier League, akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Kevin Phillips ambaye aliisimamia katika mechi 21 tofauti na 14…