Klabu ya Yanga imetoa taarifa kuwa kiungo wake Khalid Aucho raia wa Uganda amepata jeraha la mguu wake wa kushoto na atakuwa nje kwa kipindi cha wiki moja.
Taarifa hiyo inakuja kufuatia tetesi kusambaa zikidai kuwa Mganda huyo amegomea kujiunga na timu kwa kile kinachodaiwa kuwa anataka alipwe pesa zake za kusaini mkataba ndani ya klabu hiyo ambao alisaini hivi karibuni ambazo hajalipwa.
Kwa mujibu wa vipimo vilivyosimamiwa na daktari wa Yanga, Moses Etutu, Aucho hajavunjika bali ni mshipa wa mguu umevimba baada ya mshituko alioupata akiwa mazoezini.
“Mwanzo tulidhani shida ni kubwa kidogo lakini baada ya vipimo tumegundua hajavunjika bali mshipa tu umevimba, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki moja tu,” alisema Daktari.

admin
January 19, 2023

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *