
Club ya Yanga SC imemsajili kwa mkopo golikipa wao wa zamani Metacha Mnata akitokea Singida Big Stars.
Metacha anajiunga na Yanga kuongeza nguvu baada ya golikipa wao namba mbili Twalib Mshery kuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha, Yanga bado hawajatangaza usajili huo lakini kwa mujibu wa chanzo cha ndani Metacha atatambulishwa muda wowote kuanzia Jumatatu ya January 16 2023.