Benjamin Mendy amepatikana hana hatia katika mashtaka saba kati ya tisa dhidi yake.

Baada ya kesi iliyochukua takriban miezi mitano, beki huyo wa Manchester City amefutiwa mashtaka sita ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono.

Hata hivyo, baada ya siku 13 za mashauriano katika Mahakama ya Chester Crown, mahakama imeshindwa kufikia uamuzi wa mashtaka mengine mawili dhidi ya Mendy – shtaka moja la ubakaji, likihusisha mwanamke mwenye umri wa miaka 24 Oktoba 2020, na shtaka moja la kujaribu kubaka, likihusisha mwanamke mwenye umri wa miaka 29 mnamo Oktoba 2018.

Huduma ya Mashtaka ya Taji ina siku saba kuamua ikiwa itaendeleza kesi hiyo tena kwa mashtaka mawili ambapo uamuzi haungeweza kuafikiwa.

Mendy alishika kichwa chake mikononi huku hukumu zikisomwa.

Mshtakiwa mwenza wa Mendy, Louis Saha Matturie, amepatikana bila hatia ya mashtaka matatu.

Anakabiliwa na uwezekano wa kusikilizwa upya kwa mashtaka sita.

Manchester City ilimsimamisha kazi Mendy alipokamatwa Agosti 2021 na kuacha kumlipa Septemba 2021.

Mkataba wake unaisha msimu huu wa joto.

admin
January 13, 2023

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *