
Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya TFF imemuita Feisal Salum “Fei Toto” baada ya Yanga kupeleka malalamiko yake ya kimkataba dhidi ya mchezaji huyo.
Feisal ambaye anaripotiwa kuvunja mkataba na Yanga kwa kutumia kipengele kilichopo kwenye mkataba wake cha kuvunja mkataba kwa kurudisha Tsh milioni 112 ambazo ni pesa ya usajili na mishahara ya miezi mitatu.
Yanga bado hawajakubaliana na namna Feisal alivyovunja mkataba wake japokuwa kwa sasa Feisal anadaiwa kupelekwa Dubai na mmiliki wa Azam FC Yusuf Bakhressa kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kujiunga na Azam FC