Haaland hayuko katika ubora wake

Pep Guardiola anaamini Erling Haaland hayuko katika kiwango bora licha ya Mnorwei huyo kufunga mabao mawili katika ushindi dhidi ya Leeds Jumatano usiku.

Haaland, 22, alikua mchezaji mwepesi zaidi kufunga mabao 20 kwenye Premier League, akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Kevin Phillips ambaye aliisimamia katika mechi 21 tofauti na 14 za mshambuliaji huyo wa City.

Hata hivyo, kocha huyo wa Catalani anaamini kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Borussia Dortmund anaweza kuwa mkali zaidi, ingawa ana mabao 26 katika mechi 20 alizoichezea The Citizen katika michuano yote.

Guardiola, 51, alisema: “Anakosa nafasi, lakini idadi ni ya kipekee.

“Yeye ni tishio la kushangaza kwetu na kila wakati yuko katika nafasi sahihi kwa wakati unaofaa, mzuri sana.

“Nadhani bado hayuko katika kiwango bora kwa sababu ya jeraha, kucheza na mwili wake mkubwa si rahisi kwake, lakini kadri anavyoweza kucheza dakika, atakuwa bora zaidi.”

Jeraha la mguu wa Haaland limekuwa sababu ya wasiwasi kwa Guardiola na alikuwa haraka kusema kwamba anaweza kuona shida za mwili kwenye mchezo wake.

Aliongeza: “Ninahisi hayuko katika kiwango bora, ni suala la muda. Daima ni tishio la ajabu kwa mpinzani.

“Bila shaka tumefurahi, lakini kasi hiyo ndogo [ya ziada] aliyokuwa nayo mwanzoni mwa msimu, anatatizika kidogo.”

admin
December 29, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *