Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza Kijana Majaliwa Jackson aliyehusika kuwaokoa Watu 24 kwenye ajali ya ndege iliyotokea Bukoba siku jana atafutiwe kazi kwenye Jeshi la Uokozi.

Agizo hilo lililotolewa na Rais Samia kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambapo ameagiza Kijana Majaliwa Jackson akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na atafutiwe nafasi kwenye Jeshi la Uokozi ili Kijana huyo apate mafunzo zaidi kutokana na ujasiri wake huo kisha aingie kwenye Jeshi hilo ambalo linahitaji ujasiri aliouonesha.

Sasa leo Novemba 8, 2022 Rais wa Yanga Hersi akiwa Tunisia amewasiliana na Haji Manara na kuahidi kijana huyo kumpatia Pikipiki mpya itakayomsaidia kwenye shughuli zake ikiwa kama kumfariji kwa kile alichokifanya katika ajali ya Ndege iliyoanguka Ziwa Victoria.

admin
November 9, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *