Kocha Nasredine Nabi wa Yanga ameeleza mengi kuhusiana na baadhi ya watu wanahoji mfumo anaotumia huku wengine wakisema kwa nini anamchezesha Azizi Ki kama winga wakati sio winga maneno yamekuwa mengi kuhusiana na hilo.

“Mfumo unaendana na wachezaji ambao unao kwa mfano kama unaweza kucheza 4-4-2, ina maana kuna baadhi ya wachezaji hawatokuwepo unapocheza na washambuliaji wawili ina maana mawinga unawaua ili Azizi acheze kwenye huo mfumo unamrudisha kati, Feisal acheze
10, hivyo kwenye huo mfumo Azizi anacheza nusu winga sababu anatumia mguu wa kushoto ili awe anaingia katikati ila watu watahoji anamuwekaje Azizi acheze winga”>>> Nabi

“Mchezo wa mpira wa miguu unaendana na mfumo wako unaendana na wachezaji wako unavyowajua na kuangalia huu mfumo unaweza kutupata matokeo huo ndio mfumo wangu nashukuru sana sijui Kiswahili sababu ningekuwa najua ingekuwa matatizo”>>> Nabi

admin
November 9, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *