Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu kwa watu wenye ulemavu “Tembo Warriors” leo wamefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu kwa kuifunga Japan 3-1.

Michuano ya Kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu inachezwa Uturuki na sasa Tanzania itacheza robo fainali dhidi ya Haiti ambao wamefuzu hatua hiyo kwa kuifunga Marekani kwa magoli 6-2.

Tanzania sasa ina fahari kwa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, wakati Tembo Warriors wakiendelea kufanya vizuri wanasubiriwa Serengeti Girls kwenda India kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake U-17 na sasa wanajiandaa Southampton England.

admin
October 19, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *