
Klabu ya Chelsea imemtimua kocha wake Thomas Tuchel kufuatia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Dinamo Zagreb usiku wa kuamkia jana.
Wamiliki wapya wa klabu hiyo wamechagua kufanya mabadiliko kileleni baada ya kuanza kwa kigugumizi msimu huu kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Tuchel, 49, alimrithi Frank Lampard mnamo Januari 2021 na kuiongoza The Blues kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa baadaye msimu huo kabla ya kushinda European Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu(Club World Cup) msimu uliopita.
Lakini muda wake wa kuinoa umefikia kikomo kufuatia kuanza kuanza vibaya kw amsimu huu, jambo ambalo limewafanya washika mitutu hao wa London kuwa na pointi 10 katika mechi sita za Ligi Kuu ya Uingereza.
Taarifa rasmi ilisema: “Kwa niaba ya kila mtu katika Chelsea, klabu ingependa kuweka rekodi ya shukrani zake kwa Thomas na wafanyakazi wake kwa jitihada zao zote wakati wao na klabu.
“Thomas atakuwa na nafasi katika historia ya Chelsea baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa, Kombe la Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu katika wakati wake hapa.
“Wakati kundi jipya la umiliki likifikisha siku 100 tangu lichukue klabu, na huku likiendelea na kazi kubwa ya kuipeleka klabu mbele, wamiliki wapya wanaamini ni wakati mwafaka wa kufanya mabadiliko haya.
“Wakufunzi wa Chelsea watachukua jukumu la kuinoa timu kwa mazoezi na maandalizi ya mechi zijazo huku klabu ikipiga hatua za haraka kuteua kocha mkuu mpya.”
Tuchel aliungwa mkono kwa kiasi kikubwa katika soko la usajili msimu huu, huku zaidi ya pauni milioni 200 zikitumika kuwanunua mastaa kama Raheem Sterling, Kalidou Koulibaly, Marc Cucurella na Wesley Fofana.


Lakini uchezaji wao haukufikia matarajio kwani Chelsea walipoteza dhidi ya Leeds na Southampton, West Ham huku wakiwapiga kwabahati Leicester wakiwa na wachezaji 10 nyumbani wiki za hivi karibuni.
Presha ilizidi kuongezeka jana usiku kufuatia kushindwa huko Croatia.
Alisema: “Ni uchezaji duni kutoka kwetu. Tuna hadithi hizo hizo kila siku zote.
“Tumekuwa na mwanzo mzuri, hatumalizi nusu ya nafasi zetu tunazopata,tunatoka mchezoni na wakati pengine tungeweza kushinda katika dakika 15-20 za kwanza.
“Kisha shambulio moja tunafungwa, ambalo ni rahisi sana, na kutoka hapo tunakuwa na wakati mguu kimchezo.”
Alipoulizwa ni wachezaji wangapi walikuwa kileleni mwa mchezo wao, Tuchel aliongeza: “Sio wengi kwa sasa.
“Sijui uchezaji wa namna hii unatoka wapi. Ni ukosefu wa hari, nguvu, ukosefu wa nia ya kushinda pambano, kufanya mambo kwa kiwango cha juu.
“Huwezi kutarajia kushinda michezo, si katika Ligi Kuu au Ligi ya Mabingwa. Hatupo tunapotaka kuwa.”
Mechi inayofuata ya Chelsea ni safari ya majirani wa Fulham Jumamosi wakati wa chakula cha mchana na klabu hiyo imesema hakuna maoni zaidi yatakayotolewa hadi uteuzi itakapofanywa.