Club ya Azam FC imetangaza kuachana na Kocha wake Mkuu Abdihamid Moallin pamoja na msaidizi wake Omar Nasser na sasa timu itakuwa chini ya Kocha wa Makipa Daniel Cadena mwenye leseni ya UEFA Pro.

Hata hivyo Azam FC imetangaza kuwa Moallin na Omar hawataondoka Azam FC badala yake watapangiwa kazi nyingine, Azam FC hadi sasa msimu huu imecheza mechi 2, imeshinda moja na sare 1.

Uamuzi wa Azam FC unakuja ikiwa ni miezi nane impedita toka January 2022 waamue kumpandisha Moallin kuwa Kocha Mkuu, Moallin inatajwa kuwa anarudi katika nafasi yake awali.

admin
August 30, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *