Mshambuliaji wa Afrika ya Kati mwenye asili ya Congo DR Cezar Manzoki (25) amejiunga na club ya Dalian Pro ya China akitokea Vipers SC ya Uganda kwa mkataba wa miaka mitatu.

Manzoki aliyekuwa anahusishwa na Simba SC kwa kiasi kikubwa hadi uvumi kusema ameshasaini Simba SC, amejiunga na Dalian Pro kwa ada ya uhamisho ya USD 400,000 (Tsh milioni 932).

Manzoki alikuwa mchezaji bora wa Uganda 2021/2022 na alikuwa mfungaji bora pia wa Ligi Kuu Uganda msimu huo kwa kufunga magoli 18, mchezaji bora wa wachezaji na mshambuliaji bora wa msimu.

admin
August 29, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *