Siku moja baada ya Tanzania kupoteza kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu CHAN, Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetangaza kumuondoa Kocha Mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen Raia wa Denmark pamoja na Wasaidizi wake.

Poulsen anaondoka katika nafasi ya Ukocha Mkuu Taifa Stars na kusalia katika Timu za vijana hadi mkataba wake utakapomalizika.

Nafasi ya Kim itachukuliwa na Hanour Janza, akisaidiwa na Meck Mexime ambaye ni Kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar na Kagera Sugar huku Juma Kaseja ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba, Yanga na KMC akiwa Kocha wa magolikipa.

admin
August 29, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *