Afisa habari wa Yanga SC anayetumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili kujihusisha na soka pamoja na faini ya Tsh milioni 20 Haji Manara leo ametumia ukurasa wake wa Instagram na kumkosoa CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez kuwa anakosea kujisifia Simba SC kutoa wachezaji wengi timu ya Taifa Stars.

“Kuna Vitu unapokuwa kiongozi hupaswi kusema,inaleta Ukakasi na ni Ushamba, Usimba na Uyanga kwenye Timu ya Taifa ni Sumu kubwa kwenye maendeleo ya hii Timu,,tumekuwa tunaleta utimu hadi kwenye National Team na imetugharimu Kwa muda mrefu mno”

“Mengine tuwaachie Washabiki Oya Oya wa Mtaani ambao kwao kila kitu ni kutambiana tu,,lakini unapokuwa kiongozi kuna vtu hupaswi hata kuvifikiria. Last Game Wachezaji wengi waliocheza Taifa Stars,walitoka Yanga na hatukuona kiongozi yoyote wa Club hyo akitamba Kwa hilo,,Coz wanapokuwa pale,wote wanakuwa Wawakilishi wa nchi”

“Team yenyewe haipati mashabiki wengi wa kuisapoti Uwanjani ,kisha kiongozi wa Club unaleta ushabiki kisa Wachezaji wa Team yako wengi wamechaguliwa. Utajisikiaje kuona Mchezaji wa team yako akizomewa uwanjani na shabiki wa Club nyingine? Na Hilo utakuwa hujasababisha ww kwa kuandika ujinga kama huo?”

“Ni ile Basi tu mengine hatutaki kusema,,katika hao Tisa kuna wengine hata Game moja hawajacheza msimu huu,,inashangaza hata imekuwaje waitwe kwenye hiyo team. Nb; Je tukubaliane kuwa Tarehe kumi na Tatu iliyofungwa na kina Mayele ni Team ya Taifa?”

admin
August 24, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *