
KRC Genk inamkaribisha tena Ally Samatta kwenye dimba la Cegeka Arena. Makubaliano ya kukodisha yamefikiwa na Fenerbahçe hadi mwisho wa msimu wa sasa, ikijumuisha chaguo la kununua.
ZAlly alifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki kuanzia Januari 2016 hadi Januari 2020, kabla ya kuhamia Aston Villa na kuingia Ligi Kuu. Tayari ana mechi 191 akiwa Genk kwenye kaunta, ambapo alifunga mara 76 na kutoa asisti 20. Pia alikuwa na mchango mkubwa katika msimu wa ubingwa wa 2018-2019.


