
Mabingwa wa Ligi Kuu ya vijana nchini Ufaransa (U-19) club ya Montpellier wakati wakisubiri kucheza mchezo wao wa nusu fainali ya Cambiasso Tournament U-20 Ijumaa ya August 29 katika uwanja Benjamin Mkapa dhidi ya KCCA ya Uganda wametembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kwa ajili ya kufanya utalii na kujionea wanyama.



