Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ya wachezaji wa ndani leo imeshinda 1-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wao wa kwanza kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika 2023 nchini Algeria kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Tanzania imepata goli hilo kupitia kwa Abdul Seleman Sopu dakika ya 46 na itacheza tena na Somalia July 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Tanzania ikiwa nyumbani.

Leo Tanzania ilicheza Benjamin Mkapa kama timu mgeni kutokana na Somalia kuamua mechi zote zichezwe Dar es Salaam sababu hali ya usalama sio nzuri Somali, Tanzania ikimtoa Somalia itavaana na Uganda round inayofuata.

admin
July 30, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *